WEMA ABADILI NGOZI YAKE KWA SIRI...ATUMIA SH. MIL 13. HABARI ZIMEVUJA NA YEYE ATHIBITISHA...BOFYA HAPA


IMEVUJA! Kumbe ile safari ya nchini China ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ‘Madam’ lengo lilikuwa kubadili ngozi ya mwili wake katika mwonekano mpya ambayo ilishaharibika kwa mkorogo, Amani limetonywa.
Wema Sepetu ‘Madam’.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini, staa huyo aliingia nchini humo na mdogo wake aitwaye Bite ambaye kazi yake kubwa ilikuwa kufanya mawasiliano na nyumbani, Tanzania endapo lingetokea baya wakati wa zoezi hilo.
KWA NINI ALIAMUA KUDILI NA NGOZI?
Mpashaji wetu aliliambia Amani kwamba, Wema alichoshwa na ‘vijembe’ vya watu mbalimbali wakiwemo wabaya wake kuwa ngozi yake imebabuka kwa kutumia mkorogo kupitiliza.
Miguu ya Wema Sepetu ‘Madam’ kabla ya kubadili ngozi.
“Kuna wakati Wema alikuwa akikosa amani kutokana na maneno ya watu, wengine waliokuwa wakimrushia vijembe ni masupastaa wenzake, ndiyo maana akaamua kwenda China kubadili ngozi yake iwe na mwonekano mpya,” kilisema chanzo.
Habari zaidi zilidai kwamba, supastaa huyo hakupenda kabisa Wabongo wajue kuwa yupo China kubadili ngozi, hata baadhi ya magazeti yalipoandika amekwenda kujirusha na msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ alimshukuru Mungu siri yake imesitirika.
Wema.
UBADILISHAJI WA NGOZI WATUMIA SAA 12
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Wema aliingia kwenye kliniki ya ngozi katikati ya mwezi Oktoba, saa 3:12 asubuhi na shughuli ikamalizika saa 2:25 usiku.
“Alikaa kliniki toka saa tatu na dakika kumi na mbili asubuhi hadi saa mbili na dakika ishirini na tano usiku,” kilisema chanzo.
MADAKTARI WAMWONYA
Habari zaidi zinaeleza kuwa, madaktari waliokuwa wakimfanyia zoezi hilo walipomaliza walimuonya kutorudia tena kutumia mikorogo au aina yoyote ya losheni zenye kubabua ngozi, kama vile carolite.
SEHEMU ZILIZOHARIBIKA SANA
Kwenye mwili wa Wema, sehemu zenye mikunjo kama nyuma ya magoti, kukaribia makwapa, mapajani na mbele ya viwiko ndizo ziliongoza kwa kuharibika hali iliyokuwa ikimfanya mara nyingi ashindwe kuvaa sketi za vimini.
SHILINGI MILIONI 13 ZAYEYUKA
Katika zoezi hilo, Wema ambaye pia ni msanii wa filamu za Bongo na bosi wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame Production ya jijini Dar, ametumia shilingi za Tanzania, milioni 13 ikiwa ni pamoja na nauli yake na Bite kwenda China na kurudi, malazi na chakula.
APEWA DAWA YA KUZUIA KUZEEKA MAPEMA
Baada ya ubadilishaji huo wa ngozi, Wema alipewa dawa ambazo zitamsaidia kutozeeka mapema.
AONYWA MATUMIZI YA SIGARA NA KUTOLALA KWA WAKATI
Mbali na dawa hizo, staa huyo alionywa na matumizi ya sigara aina yoyote ile na kujipanga upya kwenye suala la kulala mapema ili apate usingizi wa kutosha.
MENEJA WAKE ATINGA CHINA KUHAKIKI NGOZI
Habari zaidi zikawekwa wazi kwamba, Wema alimwita meneja wake, Martin Kadinda kwa lengo la kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya staa huyo.
Juzi, Amani lilimtafuta Dk. George wa zahanati maarufu ya Sino iliyopo Sinza Mapambano (Kwawachina) ambapo alisema warembo wengi hubadili ngozi kwa mtindo wa plastic surgery, mara nyingi sehemu yenye mikunjo au kuharibika hukatwa na kuvutwa, kama mtu alishaanza kuzeeka huonekana kijana.
“Nchi maarufu kwa kubadili ngozi ni Thailand, lakini China na Afrika Kusini zimeanza  kutoa huduma hiyo.
“Hapa nchini bingwa wa masuala ya ngozi ni Profesa Masawe, zamani alikuwa Muhimbili kwa sasa ana kituo chake upanga Dar,” alisema Dk. George.
Kuhusu madhara, Dk. George alisema hayako wazi sana inategemea maisha ya mtu ya kila sikiu.
MENEJA WA WEMA AZUNGUMZA
Baada ya gazeti hili kuzinyaka habari hizo, lilimtafuta meneja wa Wema, Martin Kadinda alipoulizwa alikiri kwenda China kwa ajili ya kuhakiki mwonekano mpya wa ngozi ya ‘Beautiful Onyinye’ huyo na kusema kuwa ilikuwa lazima bosi wake afanyiwe hivyo kwa sababu bosi ni kioo cha jamii.
“Unajua Wema ni kioo cha jamii, hivyo si vyema watu kumsema kwa kitu kidogo kuhusu ngozi yake kwani hata yeye alikuwa hapendezwi nayo. Lakini nashukuru sana kwa sasa ana mwonekano mpya wa ngozi.
“Nilikwenda kuhakikisha kama ngozi yake kwa sasa inaweza kuwa na mwonekano mpya, ni kweli wamefanikiwa madaktari. Wamempa masharti kadhaa, kama kulala sana,  lakini pia wamempa dawa nyingine,” alisema Kadinda.
WEMA MWENYEWE SASA
Baada ya kuzungumza na Kadinda, Amani lilimuendea hewani Wema ili kumsikia na yeye kuhusu kubadili ngozi nchini China.
Amani: Mambo Wema, za China?
Wema: Salama tu, niambie.
Amani: Hapa kuna habari kuwa safari yako ya China ilikuwa kwa ajili ya matengenezo ya ngozi yako, vipi ni habari za kweli?
Wema: Ah! Sasa ngozi yangu imekuaje kwani?
Amani: Inasemekana una mwonekako mpya wa ngozi, ile ya kwanza hukuipenda kwa sababu ya kujeruhiwa na mkorogo.
Wema: (kimya kidogo) oke, sikupenda kulizungumzia hilo kwa sasa lakini ndiyo hivyo kama ulivyosikia.
Amani: Unaweza kuniambia ni shilingi ngapi umetumia?
Wema: Mh! Mbona unanikaba koo jamani? Kama shilingi milioni 13 pamoja na gharama za usafiri.
Amani: Nashukuru sana Wema.
Wema: Karibu sana.

TAZAMA LULU ALIVYO FANANA NA BIBI YAKE [COPY RIGHT]

LULU MICHAEL NA BIBI YAKE
Mwigizaji maarufu na wa filamu na maigizo ya kibongo Lulu amepiga picha hiyo na bibi yake  mzaa mama baada ya  bibi huyo kuja dar es salaam kumtembelea mwanae {mama wa lulu} na wajukuu zake.
Eti wanafanana toa maoni yako hapo chini

TAZAMA HOMA YA FIESTA ILIVYO MFANYA DIAMOND PANDE ZA LEADERS



Staa wa Bongo Fleva,Nasib Abdul,Diamond Platinumz ametembelea pande za Leaders Club na kuona jinsi maandalizi ya jukwaa la serengeti Fiesta likiendelea na kuwaambia mashabiki kuwa ataangusha bonge la shoo kama kawaida yake na mashabiki waende kushuhudia tu siku ya Jumamosi Oct.26.
Pia kupitia mtandao Diamond aliandika kuwa.....Kwa heshima ya Mashabiki zangu Nchi na Taifa langu ilinibidi nirudi Maalumu kabisa kwajili ya Shoo hii ya Fiesta Jumamosi pale Leaders Club ili kuwakaribisha wageni zetu toka nje... lakini pia kuwadhihirishia Wageni Hao kuwa Tanzania si ya legelege imebarikiwa Wasanii na wenye uwezo...! Tukutane pale…
Staa wa Bongo Fleva,Nasib Abdul,Diamond Platinumz ametembelea pande za Leaders Club na kuona jinsi maandalizi ya jukwaa la serengeti Fiesta likiendelea na kuwaambia mashabiki kuwa ataangusha bonge la shoo kama kawaida yake na mashabiki waende kushuhudia tu siku ya Jumamosi Oct.26.
Pia kupitia mtandao Diamond aliandika kuwa.....Kwa heshima ya Mashabiki zangu Nchi na Taifa langu ilinibidi nirudi Maalumu kabisa kwajili ya Shoo hii ya Fiesta Jumamosi pale Leaders Club ili kuwakaribisha wageni zetu toka nje... lakini pia kuwadhihirishia Wageni Hao kuwa Tanzania si ya legelege imebarikiwa Wasanii na wenye uwezo...! Tukutane pale leaders on saturday Madau wangu...


Picha, Ney Wa Mitego Akiwa Sero kisha afunguga kilicho msibu



 
Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.

Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.

PICHA ZA MAPOKEZI YA MAHOMBI UWANJA WA NGEGE "Dar" NI KUFURU


Posted by Teen Newz on October 25, 2013 at 12:53pmComments 


View as"ej fashionrealmedia" after few minutes for more photos for arrival of international artist coming for fiesta ,itakayo happen 26.10.2013....

HASHEEM THABIT ATUMIKIA KIFUNGO KILICHO MKABILI

                                                       tazama video ya tukio hilo

    Mchezaji kikapu maarufu toka Tanzania Hasheem Thabit anaechezea timu ya kikapu  itwayo Oklahoma  inayoshiriki ligi kuu ya mpira wa kikapu ya Marekani,hatimaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kutocheza  mechi moja na kukatwa mshaara na timu yake baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa timu ya New Orleans katika mchezo ulio kutanisha timu hizo ambapo timu ya New Orleans iliibuka naushindi wa vikapu 105 thidi ya 105.

PICHA ZA HAPPY BIRTH DAY YA AMBER ROSE AKIWA NA WIZ KHALIFA mMH


 
Amber Rose Akiwa Na Mume Wake Wiz Khalifa, Wamesherekea Siku Ya Amber Ya Kuzaliwa Pamoja. Fahamu kuwa Amber Rose amezaliwa siku moja na mchumba wa x Boy Friend wake Kanye West ambaye ni Kim Kardishian, Wote wamezaliwa 21 October. Pamoja na kuwa na majukumu ya ziara za muziki Wiz Khalifa ameweza kupata nafasi ya kuwa na baby mama wake kwenye birthday yake.


HAWA NDIO VIGOLI WAPYA TISHIO LA WANAMUZIKI WA BONGO FLAVA

Classic girls interviewed by Mishery&Jenje{presenters}
                                     
                                                            Florah
                                                          Menina
                                                    Clasiic girls togethetr
                                                      classic girls performing
                                            Classic girls with the production crew
Classic girls ni moja la kundi linalo fanya vizuri katika tasnia ya muziki hasa muziki waufanyao wa kizazi kipya yani bongo flava,ambapo ili pata nafasi ya kufanya interview na kipindi cha mastaa maarufu kwa jina la STAR'S TALK hivi karibuni.Kundi hilo linalo jumwisha wasichana  wawili wakiwa chini ya meneja wao Abdallah Mziray limekuwa likija juu kwa kasi likifanya vizuri na  single tatambazo ni  kulabata, na nakataa,kwamengi zaidi katayari kwa video ya interview hio www.ejfashionrealmedia.blogspot.com na www.dar29.blogspot.com hivi karibuni USIKOSE!!

TAZAMA SALAMA JABIR ALIVYO WATUKANA WASHIRIKI 20 WA EPIQ


** *Mtangazaji wa Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia kituo cha EATV Salama Jabir, wa pili kutoka kushoto akidauiwa kutukana kwa kutumia ishara ya kidole wakati walipokuwa kwenye moja ya haraka za kurekodi matukio ya kipindi cha EPIQ BSS 2013, kinachorushwa hewani kupitia kituo cha TBC1, Salama alifanya kituko hicho akiwa ameketi mezani na Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Bongo Profesa Jay wa kwanza kutoka kushoto,mratibu wa Shindano la Bongo Star Search Madame Lita katikati na Master Jay.* 

CHEKI GARI ANAYOTUMIA NICK MINAJ SASA NI NOMA SANA



 
Nicki Minaj ni msanii asiye na aibu ya kusema mambo gani anapenda kwenye maisha yake na yupo tayari kufanya nini kuyapata. Hivi karibuni alikuwa kwenye duka la K Mart akizindua nguo zake na aliwasili na gari yake mpya iliyo tengenezwa na kuboreshwa kwa matakwa yake, Yes ndio hio Pink lamborghini Custom made for Minaj.
Picha Zaidi Ziko Hapa.