JIONEE SHILOLE ALICHO AMBULIA BAADA YA KUANDIKA KINGEREZA MTANDAONI


Shilole aliamua kutandika yai kwenye Instagram, ili kuzipa uzito shukrani zake za dhati kwa muongozaji wa video yake ya ‘Nakomaa na Jiji’ itakayotoka Jumamosi hii, Nisher.
Bahati mbaya, yai lake lilivunjika mapema wakati lilipokuwa likiufikisha ujumbe huo na kuwafanya watu waligeuzie mjadala.
Kama tumekuacha kwa lugha hiyo, ni kwamba Shilole aliandika Kiingereza kilichokosewa sarufi aka Broken English.

Shilole aliandika: I did ever think I would do a nice video like this thank you alot to my director @nisherbybee.

Baada ya hapo, haya ndio yaliyosemwa:
    [ @ ] nicrac1914 Lugha za majahazi!! Ongea Kiswahili tu utaeleweka vzr

    [ @ ] lisammbando Speaking English is not a joke Hahahahah 

    [ @ ] clararobinso Me cjaelewa hiyo lugha mpz, kwan ulitaka kuandika nn hapo?

    [ @ ] pinnadelicious Jmn mbona mnapenda kumcritisize hvo mwenzenu sa amekosea nn nyie mnaojua, duh dis is too much 

    [ @ ] teddybebe Jaman all in all si mmemuelewa.hata mbuyu ulianza kama mchicha kila kitu kinaitaji mazoezi na usione aibu hata wakikucheka mpenz jitahid tu utaelewa. @shilolekiuno 

    [ @ ] teddybebe Kumbukeni hata nyie mlitoka huko hata kama mlisoma za kishuaa. Vizur kumsahihisha na sio kumbeza  4h

[ @ ] m_bongo her message sent, delivered, read and understood hicks. By the way english isn't her first language.

    [ @ ] tutupahamidu Did or didnt?!!thank you or thanks to my director?!

    [ @ ] raqey_unique Yeah her English is not gud but a bet u all understood wat she meant so stop hating

      [ @ ] pinnadelicious Kiswahili every one anajua so mdada wawatu anajitahidi awe internationally so km tumeelewa wat she mean mbona hakuna tatizo, sema bongo tumemeza!!!!

    [ @ ] eshyleta bora washushuliwe tu, coz baadae wanaleta nyodo za kiswanglish, et kiswahili hawezi baadhi ya maneno, km huwezi kithungu tumia lugha yako ya taifa

    [ @ ] makavlive @shilolekiuno mwisho wa ujuaji ni aibu...ona sasa, ungeandika kiswahili isingekua shida, kutaka ung'eng'ee shule yenye hujaenda...acha kuiga paka la baa wee ongea kinyamwezi unachokijua!

    [ @ ] auma_bebe we al knw dat english iz not our mothertongue n tz nxma mnaijua histry yke shilole ss y mnamponda hvyo bdala hta ya kumrekebisha? sio fair bna...
 

TAZAMA MCHUNGAJI MAARUFU ANAETOA MAPEPO SEHEMU ZA SIRI

Huu sio mchezo wa kuigiza wala sio utani imetokea huko nchini Nigeria,ambapo nguvu za giza zimezidi sana,hivyo mapepo ,mashetani na hata maruwani yamekuwa ndani ya watu huku wachungaji wakifanya maombi kuyatoa mapepo na mazingara hayo kwa watu.Sasa hio picha hapo juu ni moja ya picha ilioshangaza maana mchungaji maarufu nchini  humo huyo amekuea akiombea watu uku akiwashika sehemu za siri.

WEMA AIPASUA BONGO MUVI BAADA YA KUSUSIWA MSIBA WA BABA YAKE.



KLABU ya mastaa wa filamu jijini Dar es Salaam, Bongo Movie ‘Bongo Muvi’ imepasuka katikati kisa kikidaiwa kuwa ni lile tamko linalodaiwa kutolewa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Vincent Honorati Lasasi Kigosi ‘Ray’ kuwa mwanachama yeyote wa kundi hilio asitie miguu kwenye msiba wa baba mzazi wa mwenzao, Wema Sepetu, marehemu Balozi Isaac Sepetu.
Tukio hilo la katazo lilitokea wakati wa maombolezo ya kifo cha mzee Sepetu kilichotokea Oktoba 27, mwaka huu katika Hospitali ya TMJ kwa ugonjwa wa kisukari ambapo msiba ulikuwa nyumbani kwake, Sinza Mori jijini Dar es Salaam.
LAWAMA ZOTE KWA RAY
Kufuatia madai hayo, baadhi ya wasanii wa Bongo Muvi (majina tunayo) wamekuwa wakitoa lawama zao kwa Ray huku wengine wakidai wamejitoa kwenye kundi hilo kwa sababu halina umoja na limejaa unafiki.
Maneno hayo yalianza kusambaa baada ya Wema kumaliza kumzika baba yake Oktoba 31, mwaka huu mjini Zanzibar.

  
RAY AAGIZWA AITISHE KIKAO CHA DHARURA KUMJADILI
Habari za uhakika zinasema kwamba, wasanii waliotangaza kujiengua klabuni humo wameshamuomba Ray aitishe kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumzia hatua yake ya kuwapiga marufuku wasanii hao kutoshiriki msiba wa mzee Sepetu huku akijua wema wa binadamu unapatikana kwenye kushiriki mazishi ya wenzake.
“Kikubwa zaidi ni kwamba, Ray wakati akisambaza zile meseji alisahau kuwa kuna siku Wema aliwahi kuwaalika wasanii wa Bongo Muvi nyumbani kwake Makumbusho (Dar) wakala na kunywa, mbona hawakugoma kwenda?” alihoji staa mmoja aliyepinga katazo la Ray.

NJAMA ZA KUINGAMIZA KABISA BONGO MUVI ZAUNDWA CHINI KWA CHINI
Habari zaidi kutoka kwenye kundi linalodaiwa kujimega kwenye mpasuko huo zinasema kuwa kuna njama za makusudi za kuiangamiza klabu hiyo kwa kuwa mbali na mwenyekiti huyo kuwazuia wajumbe wasiende msibani kwa mzee Sepetu lakini imekuwa ikiendeshwa kitemi na kibaguzi.
Ilisemakana kuwa kuna wasanii wameifanya klabu hiyo kama yao huku wengine wakiwa hawatakiwi hata kukohoa jambo walilosema si sawasawa.
“Kwa mpasuko huu, wasanii waliochukizwa na Ray wamesema nao wao wanakazia hapahapa, Bongo Muvi lazima iangamie moja kwa moja, isiwepo tena,” alisema msanii mmoja ambaye jina lake linapanda kwa kasi.
KISINGIZIO CHA WASANII WANAFIKI CHAPINGWA
Maumivu makali zaidi yaliibuka kufuatia baadhi ya wasanii waliotaka kujifanya hawajapata meseji ya Ray ambapo walisema walishindwa kushiriki msiba huo kwa sababu walikuwa ‘shooting’.
“Kuna wasanii walishindwa kuweka wazi kwamba walipokea meseji ya katazo ya Ray, walipopigiwa simu na wenzao kuulizwa kwa nini hawaonekani msibani kwa Wema walisingizia eti wako location wanarekodi!
“Kwa akili za kawaida, mwenzenu kafiwa mnaweza kushikwa na ubize wa kurekodi filamu? Hawa ni wanafiki, walisingizia vile ili ionekane wana hudhuru,” alisema staa mwingine.
MAMA WEMA ASHTUSHWA
Akizungumza na waandishi wetu kwa mara ya kwanza baada ya kusikia mwanaye alisusiwa msiba wa baba yake, mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu alionesha kusikitishwa sana na kitendo hicho.
Alisema kitendo hicho kilitokea wakati ambao Wema au familia nzima ilikuwa inasaka faraja na si mfarakano kwa vile kufiwa kupo na hakuna dalili wala kujiandaa.
“Nilisikitika sana, lakini siwezi kusema mengi kwa sababu vijana wanataka mwongozo ili kwenda mbele, naamini watakaa na kuondoa tofauti zao,” alisema mama huyo mwenye mapenzi makubwa na mastaa wa filamu Bongo.
KATAZO LA RAY 
LILISIMAMIA HIVI
Habari kutoka chanzo chetu makini zilidai kuwa hoja dhaifu iliyotumiwa na Ray ni kwamba Wema huwa haendi kwenye misiba ya wenzake hivyo walitaka na yeye amzike baba yake mwenyewe.
MISIBA ILIYOTOLEWA MFANO
Ulitolewa mfano msiba wa aliyekuwa staa wa filamu za Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia Januari 2, mwaka huu ambapo Wema alishindwa kufika kwa sababu alikuwa studio akirekodi wimbo wake mpya ambao haujatoka hadi leo.
MISIBA ALIYOSHIRIKI
Ilidaiwa kuwa Wema huwa hashiriki misiba ya wenzake, ikatolewa mifano misiba miwili aliyoshriki kuwa ni marehemu Sharo Milionea (Hussein Mkiety) na (Steven) Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake.
ANACHOSIMAMIA WEMA
Akizungumzia tukio la kususiwa msiba wa baba yake, Wema alifunguka:
“Nimesikitishwa na kitendo hicho naamini hakikuwa cha haki, mimi nimekuwa nikihudhuria misibani kwa watu mbalimbali na si kweli kwamba niko kivyangu, nimehukumiwa bure.”
RAY AINGIA ‘PANGONI’
Juzi Jumanne, Amani lilimsaka Ray kwa njia ya simu ili aelezee ukweli wa madai hayo lakini aliingia ‘pangoni’ (hakupokea simu).
Hata hivyo, katika gazeti ndugu la hili, Ijumaa la Ijumaa, Novemba Mosi, 2013 ukurasa wa mbele ambapo kuna habari yenye kichwa; WEMA SEPETU ASUSIWA MSIBA, Ray aliulizwa kuhusu madai hayo ambapo alijibu:
“Mh! Kweli Wema haendagi kwenye misiba ya watu, hata mimi sikumuona kwa Sajuki ingawa sijui kama alionekana baadaye ila kwa sasa niko sehemu mbaya nitakupigia baadaye tuongee kwa kirefu.”
Hakupiga.
MASTAA KIDUCHU MSIBANI
Pamoja na katazo hilo la Ray, wasanii wengine waliamua kwenda msibani Sinza – Mori (Dar) na wachache sana kwenye mazishi, Zanzibar.
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Kajala Masanja, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Jacob Stephen ‘JB’, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, Salum Mchoma ‘Chiki’, Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na Jacqueline Wolper.
WASIOFIKA MSIBANI 
Wengi walimsusia msiba Wema, lakini majina makubwa zaidi wakiongozwa na Ray mwenyewe ni Single Mtambalike ‘Richie’, Steven Mengele ‘Steve Nyerere’, Irene Paul, Blandina Chagula ‘Johari’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’ na Ruth Suka ‘Mainda’
Chanzo:GPL
-----------

SOMA HAPA JIPYA TOKA KWA WALTER CHILAMBO ,YAN NI SHiiiidaaaa


Soma Hapa Post Ya Walter Chilambo Kuhusu Kazi Mbili Mpya Kutoka Kwake.




HUU NDIO MUINEKANO MPYA WA WEMA SEPETU BAADA YA MSIBA WA BABA YAKE

Wema sepetu na nduguzake
Wema ni mzuri ata akiwa kwenye majonzi.

TAZAMA KILICHO TOKEA KATIYA WEMA NA JOKATE KWENYE MSIBA WA BABA WEMA

Warembo wa wili wenye umaarufu nchini na nje ya nchi ya tanzania  wanaotambulika kwa majina Wema sepetu na Jokate Mwegelo ,ambao urafiki na ujirani wao ulipotea baina yao hivi kwa mdaa sasa baada ya sakata lao kuchukuliana bwana " DIAMOND PLUTINUMZ".Ila baada ya msiba wa baba mzazi wa wema sepetu Jokate aliuzuria msiba huo kulingana na maelezo ya maneger wa Wema sepetu ambaye ni Martin Kadinda, alisema" nimefurahi na kustajabu kumuona jokate akijumuhika nasi katika msiba wa baba yetu mzee Abraham Sepetu maana ajawahi shirikiana nasi kwa muda mrefu sana sasa"hivyo msiba huo umeweza wakutanisha warembo hao.

TAZAMA PICHA ZA MWANAFUNZI ALIE JINYONGA KWA SABABU YA MTHIANI 2013

Mwanafunzi alijinyonga siku moja kabla ya mthiani wa taifa wa kidato cha nne alie julikana wa jina la Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata.

Mwenyekiti  wa serekali ya Mwangata C Bw salehe Mwingwa akiisoma barua ilioandikwa na kuachwa nakijana huyo yenye ujumbe wa sababu ya yeye kujinyonga ambayo ni uwoga wa mthiani wa taifa wa kidato cha nne 2013.

PICHA ZA ALICHOKIFANYA MTOTO KWA PAPA FRANCIS WA PILI, SIOKAWAIDA



Mtoto moja asiejulikana kwa jina  alionyesha furaha yake huku akishangaza watu  baada ya kumvamia PAPA FRANCIS 2 nakumkumbatia kisha akaendelea kucheza  huku papa huyo akiendelea kuhutubia haikuishia hapo mtoto huyo akaenda  kekaa kwewnye kiti special/maalumu cha papa huyo kiongozi wa dini ya wakristowa roman diniani.