ronaldo copyMichuano ya kombe la dunia imeendelea kuonyesha ukubwa wake kwa kuteka kila habari kuu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mabilioni ya watu duniani kote wakiwemo mastaa wakubwa wa kitaifa na kimataifa  wanafuatilia michuano hii ambayo ndio mikubwa kabisa katika soka duniani. 


10402904_752093688187912_8259365943125327229_n-1
Mmoja wa mastaa wa kibongo ambaye ameonyesha kufuatilia michuano hii pamoja na wachezaji shiriki ni Jokate Mwegelo, ambaye mtangazaji wa TV, muigizaji na mmiliki wa lebo mavazi na fashion kiujumla ya Kidoti.
Tangu kuanza kwa michuano hiyo Jokate amekuwa akiposti posti tofauti kuhusiana na michuano hiyo, huku akionyesha namna anavyomkubali mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo, mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno inayoshiriki kwenye kombe la dunia mwaka huu.
“Ronaldo ni mchezaji mzuri, anajituma uwanjani na anafunga magoli akiisadia timu anazochezea. Ana nidhamu ya kazi yake na akiifanya anaifanya kiuhakika na ndio maana tangu akiwa Manchester United nikajikuta namshabikia. Pamoja na hayo kitu kingine ambacho kinanifanya kumkubali Ronnie, ni namna ambavyo anajitoa kusaidia watu wasiojiweza, kama tulivyosikia juzi ametoa kiasi cha zaidi ya millioni 100 za kitanzania kusaidia matibabu ya mtoto aliyekuwa na matatizo fuvu la ubongo kujaa damu.”
10473394_249343711920920_4954243716833458720_nAkizungumzia michuano ya kombe la dunia, Kidoti alisema, “Kwenye michuano hii nilikuwa nasapoti timu za Afrika lakini zinaniangusha, hazichezi vizuri. Pia naisapoti Ureno kwa sababu ya nampenda Ronaldo, na Brazil pia nawapenda wanacheza vizuri hasa yule Neymar. Van Persie pia namkubali, lile goli alilofunga dhidi ya Spain kwa kichwa, aisee ni moja ya magoli bora kabisa.”
 
Top