Msanii maarufu wa miondoko ya Bongo fleva Bob Juniour maarufu kama "rais wa masharobaro" akiri kuwa mziki umechangia kwa asilimia kubwa kuvunjika kwa ndoa yake.Rais huyo wa Masharobaro ambae ni mmiliki pia ni producer wa lebo ya Sharobaro Records inayopatikana Magomeni Mapipa,alitamka hayo katika kipindi cha Star's Talk Tz kinachoandaliwa na E j Fashion & media kwa ushirikiano na blog ya Dar29  na kudai kuwa mkewe alishindwa kuvumilia simu za warembo ambao ndio idadi kubwa ya washabiki wake,zilizokuwa zikiingia mara kwa mara.Pia Bob Junior  ambae ni baba wa mtoto mmoja (1) wa kiume alidai picha alizokuwa akipost kwenye mitandao ya ki jamii na comment zilizokuwa zikitolewa na mashabiki wake zilimgombanisha na mtalaka wake.


  Bob Junior mwenye ngoma mpya hivi sasa inayoitwa "Bashasha" alioshirikisha Vanessa Mdee ambayo imeanza kuteka mashabiki wa Bongo fleva katika vituo mbalimbali vya redio nchini kote, kasema kuwa video ya ngoma hiyo iko karibu na itafanywa na kampuni  Ogopa Video kutoka nchini Kenya.
Video ambayo amedai itakuwa moto wa kuotea mbali huku akimalizia kwa kusema "Rais akipita kaa kimya".
 
Top