Matukio mbalimbali ya sherehe hiyo katika picha.
Wageni waalikwa wakiwa ndani ya ndege wakielekea Florence, Italia kwa ajili ya ndoa ya Kim na Kanye.
Ukumbi wa Chateau De Versailles ambalo wageni waalikwa walikuwa wakisherehekea maandalizi ya harusi toka jana.
Kim Kardashian (katikati) akiwa na ndugi zake muda mfupi kabla ya kusafiri kwenda Florence, Italia.
Wageni waalikwa wakisheherekea maandalizi ya harusi jana usiku.
Dada wa Kim, Kourtney Kardashian akiwa na mumewe, Scott Disick.
Jengo la Hall of Mirrors, moja ya jengo ambalo wageni waalikwa walikuwa wakisheherekea maandalizi ya ndoa.
Kim na Kanye wakijiandaa kuelekea kwenye gari tayari kwa kufika uwanja wa ndege na kusafiri kwenda kufunga ndoa.
Wakati leo ndiyo siku ya harusi ya rapa Kanye West anayemuoa Kim Kardashian katika sherehe itakayofanyika Florence nchini Italia, msanii huyo wa kiume amesema mkewe mtarajiwa ni mzuri kuliko kipaji chake.
Jumla ya wageni 600 walikuwepo katika pati maalum iliyofanyika jana katika ukumbi wa Hall Of Mirrors ambako wawili hao walithibitisha kufanyika kwa ndoa yao leo.
Hata hivyo, katika sherehe hiyo, Best Man, Jay Z na mkewe Beyonce hawakuwepo, ingawa bvado kuna matumaini kuwa wapambe hao wa karibu wa wanandoa watarajiwa, watakuwepo harusini baadaye leo
 
Top