Kumeibuka kikundi kinachojiita ‘Destroy the Innocents’ a.k.a ‘DI’ ambacho kazi yake kubwa ni kuchafua watu mitandaoni kwa faida zisizojulikana na tayari Miss Tanzania namba mbili, 2006/07, Jokate Mwegelo, ameshughulikiwa na kundi hilo kiasi cha kukesha akilia wiki nzima.


Joketi, mrembo ambaye amekuwa akijitahidi sana kujiepusha na kashfa na mpaka sasa hajakumbwa na ‘skandali’ yoyote ‘siriasi’, kwa wiki nzima, sasa amekuwa akilia baada ya picha ya msichana anayeaminika kuwa ni yeye, kubandikwa mtandaoni (hatuutaji mtandao), kama inavyoonekana ukurasa wa mbele kulia, akifanya ngono na mwanaume asiyejulikana.

Picha hiyo inayomwonesha Jokate akifanya ngono mtandaoni, hivi sasa imesambazwa kwa nguvu zote kwenye simu za watu kupitia utaratibu uitwao Blue Tooth na Memory Card, ikisemekana lengo ni kuendelea kumchafua mnyange huyo, ambaye siku zote amekuwa akionekana mwema na mwenye sifa nzuri mbele ya jamii.

Kama kawaida, gazeti hili lilikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kabisa kuinasa picha hiyo kwa sababu hushughulika sana na skendali za watu maarufu, ambapo katika kikao cha gazeti, picha hiyo ilipokelewa na kuanza kuchunguza vizuri kipande hicho cha video na mabishano makubwa kutokea, huku baadhi ya wajumbe wakisema “Ni Jokate na wengine wakisema siyo”!

Kilichomwokoa mrembo huyo na kuonyesha kuwa picha hiyo si yake bali ni ya msichana anayefanana nae sana, ni kidude cheusi (love spot), ambacho Mungu alimwekea Jokate juu ya mdomo wake wake, (kama kilivyozungushiwa kiduara chekundu katika picha halisi ya Jokate iliyoko kushoto ukurasa wa mbele), alama ambayo hakika, ndiyo iliyookoa heshima ya yake iliyokuwa hatarini kutoweka.

Picha ya msichana aliyewekwa mtandaoni akifanya ngono haina kidoti hicho cheusi ambacho kimekuwa alama ya Jokate, hivyo kufanya kile kinachofanywa na Kikundi cha Destroy the Inocent, kuonekana ni uongo wenye lengo la kumchafua mlimbwende huyo.

Ni tofauti ya picha hizo mbili, ndiyo iliyofanya gazeti hili na mengine mengi kutochapisha habari hiyo, baada ya kuthibitisha kuwa, kashfa hiyo ni uongo unaofanywa kwa lengo maalum na kundi hilo chafuzi.

Gazeti hili linalaani kitendo kinachofanywa na Kikundi cha Destroy the Innocents cha kuchafua majina ya watu kwa makusudi na juhudi zinaendelea ili kuwanasa watu hao kwa lengo la kuwafikisha mikononi mwa sheria, huku ikidaiwa kuwa, baadhi yao ni wanafunzi wa Chuo Kikuu kimoja maarufu jijini Dar es Salaam.


 
Top