Mwanamitindo na mwigizaji asiyekaukiwa vituko wa Marekani Amber Rose alitua hivi karibuni nchini Nigeria na kuwa jaji katika shindano la kumsaka mrembo wa Miss Earth 2013 ambapo mrembo Marie Miller aliibuka mshindi na kuvishwa taji.
Pamoja na Amber Rose pia na Mwana hip hop Karlie Redd na mwigizaji wa nchini Marekani Boris Kodjoe waliohudhuria shindano hilo liliokuwa na msisimko mwa aina yake huku watu wengi waliohudhulia shindano hilo walityaka kujua Amber angevaa nini.
Tukio hilo lilifanyika katika Hoteli ya Mashariki, Lagos ambapo Amber Rose alitupia kigauni kifupi cha rangi ya cream na koti jeusi na viatu virefu vyeusi huku akikamilisha kwa pete ya almasi na kukata nywele zake kwa staili ya kipekee.
Ambapo kwa upande wa Boris Kodjoe aliwasili katika ukumbi kwa mtindo wa sartorial.
 
Top